Jermeri (kwa Kifaransa: Germier; aliishi karne ya 6 au karne ya 7) alikuwa kwa miaka minne askofu wa Toulouse nchini Ufaransa ambaye alijitahidi kutembelea waumini wake na kuinjilisha bonde la mto Garonne[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi[2] kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Mei[3].