Kikutep

Kikutep ni lugha ya Kiniger-Kongo nchini Nigeria inayozungumzwa na Wakutep. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kikutep nchini Nigeria imehesabiwa kuwa watu 44,600. Pia kuna wasemaji 1400 nchini Kamerun. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikutep iko katika kundi la Kijukunoidi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne