Kilamba

Kilamba ni lugha ya Kibantu nchini Zambia inayozungumzwa na Walamba. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kilamba imehesabiwa kuwa watu 219,000. Pia kuna wasemaji katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kilamba iko katika kundi la M50.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne