Kinaro

Kinaro (au Kinharo) ni lugha ya Khoisan nchini Namibia na Botswana inayozungumzwa na Wanaro. Mwaka wa 2014 idadi ya wasemaji wa Kinaro nchini Botswana imehesabiwa kuwa watu 8000. Pia kuna wasemaji 4000 nchini Namibia (1998). Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kinaro kiko katika kundi la Kikhoe.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne