Kiratahan

Kiratahan ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Waratahan kwenye kisiwa cha Sulawesi. Mwaka wa 1999 idadi ya wasemaji wa Kiratahan imehesabiwa kuwa watu 500 tu, na tangu pale, idadi imepungua tena sana, yaani lugha ya Kiratahan imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiratahan iko katika kundi la Kifilipino.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne