Rika

Rika ni kundi la watu katika jamii ambao wana umri uliokaribiana na hupitia pamoja mivigha au hatua za maisha.

Mifumo ya marika ilikuwa (na pengine bado) ni kawaida katika makabila mbalimbali ya Afrika Mashariki, kwa mfano Wanyakyusa, na Afrika Kusini, kwa mfano Wazulu. Mifumo hii ilitumiwa katika tohara, majeshi na utawala[1][2].

  1. Keesing, R. M. 1981. Cultural Anthropology: A Contemporary Perspective (2nd ed.). New York: Holt, Rinehart and Winston. ISBN 0-03-046296-7.
  2. Dyson-Hudson, Neville. 1963. "The Karimojong Age System." Ethnology 2: 353-401.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne