Bahati

Jani linalodhaniwa kuleta bahati njema.

Bahati (kutoka neno la Kifarsi/Kiajemi "bakht", بخت; pia: sudi; kwa Kiingereza: lucky) inatafsiriwa kwa namna tofauti.

Kwa mfano, Kamusi ya Noah Webster inafafanua bahati kama "nguvu isiyo na lengo, isiyotabirika na isiyotawalika inayosababisha matukio mazuri au mabaya kwa mtu binafsi au kundi la watu".[1]

Kumbe Max Gunther inatafsiri hivi: ni "matukio ambayo yanaathiri maisha ya mtu na yanaonekana kuwa nje ya udhibiti wake".[2]

Uwepo wa bahati unasadikiwa au kukanushwa kadiri ya utamaduni, falsafa, dini na hisia za watu. Kwa mfano Ukristo unafundisha Maongozi ya Mungu ambayo yanategemea Hekima yake, si bahati nasibu.

  1. Gunther, 1977. View on Google Books.
  2. Ibidem, Gunther, 1977.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne