Hekima

Mapembe kichwani mwa Musa alivyochongwa na Michelangelo ni kielelezo cha hekima.
Sanamu ya hekima katika Ugiriki wa kale kwenye Celsus Library huko Efeso, Uturuki.

Hekima ni hali bora ya mtu katika kutambua ukweli wa binadamu, vitu, matukio na mazingira mbalimbali hata kuchagua vizuri la kufanya.

Katika dini mbalimbali inatokana na imani kwa Mungu.

Katika Ukristo inatajwa pengine kati ya vipaji vya Roho Mtakatifu vinavyokamilisha maadili ya kiutu na maadili ya Kimungu vilevile.

Ndicho kipaji bora ambacho hutusaidia tupende na kufurahia mambo ya Mungu.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne