Karanga

Kwa matumizi mengine ya jina hili angalia Karanga (Moshi Mjini)

Karanga zilizokauka

Karanga au njugu (kwa Kiingereza: peanut au groundnut) ni mbegu ya mnjugu na moja kati ya mazao muhimu duniani. Jina la kisayansi la mmea huo ni Arachis hypogaea.

Vikonyo vya karanga vinaingia katika ardhi na makaka yanaiva hapa chini. Baada ya kukauka makaka haya na matunda ndani yao hufanana na jozi kwa hiyo kuna majina kama "jozi ya ardhini" katika lugha mbalimbali[1] .

Karanga zinaliwa moja kwa moja, hasa baada ya kukaangwa, zinasagwa kuwa siagi ya karanga na hasahasa zinasagwa na kukandamizwa kwa kupata mafuta ya karanga kwa upishi au matumizi viwandani. Mabaki ya karanga baada ya kutolewa kwa mafuta ni lishe bora la nyongeza kwa mifugo kama ng'ombe.

Karanga au mafuta yake vinaweza kusababisha mzio kwa asilimia ndogo za watu lakini hili ni tatizo katika nchi ambako chakula ni hasa chakula kilichoandaliwa viwandani kutokana na matumizi mapana ya karanga.

  1. ing. groundnut, jer. Erdnuss, hol. aardnoot, far. بادام زمینی badam zamini, lakini Kiafrikaans grondboontjie "maharagwe ya ardhini"

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne