Kichwa

Mchoro wa kichwa cha binadamu

Kichwa ni sehemu ya mwili ambayo kwa mwandadamu na vetebrata huwa na ubongo, macho, masikio, pua na kinywa ambazo hutumiwa kwa kuona, kusikia, kunusa, na kuonja.

Kichwa ni sehemu iliyo tofauti na kiwiliwili. Maumbile ya kichwa yametokea kwa njia ya mageuko ya uhai. Katika mchakato huu milango ya fahamu, mdomo na kitovu cha neva zilianza kukaa pamoja kwenye sehemu ya mbele ya viumbe. Kwa vertebrata mkusanyo huu umepata kinga cha mifupa ya fuvu kinachviringisha mkusanyiko wa neva ulioendelea kuwa ubongo.

Kwa binadamu kichwa huwa kimefunikwa na nywele.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne