Kihindi

Kihindi (Devanagari: हिन्दी au हिंदी) ni lugha ya Kihindi-Kiulaya nchini Uhindi, Nepal, Afrika Kusini na Singapuri inayozungumzwa na Wahindi. Ni lugha ya kitaifa nchini Uhindi. Mwaka wa 2001 idadi ya wasemaji wa Kihindi nchini Uhindi imehesabiwa kuwa watu milioni 258; tena kuna watu milioni 120 ambao huitumia lugha ya Kihindi kama lugha ya pili au ya mawasiliano. Wengine husema kwamba kinaeleweka kati ya theluthi mbili ya Wahindi wote yaani takriban watu milioni 650, na wasemaji wa Kihindi kama lugha ya kwanza ni zaidi ya milioni 180. Pia kuna wasemaji 361,000 nchini Afrika Kusini (2003), wasemaji 77,600 nchini Nepal (2011) na wasemahi 13,100 nchini Singapuri (2010). Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kihindi iko katika kundi la Kiaryan au la lugha za Kihindi-Kiajemi. Lugha za karibu ni pamoja na Kipunjabi, Kisindhi, Kigujarati, Kimarathi na Kibengali.

Lugha imetoka katika Sanskrit ya kale iliyokuwa lugha ya chanzo cha utamaduni wa Uhindi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne