Methali

Methali (kutoka neno la Kiarabu مثل mathal) ni usemi mfupi wa mapokeo wenye mpangilio maalumu wa maneno unaodokeza kwa muhtasari fikra au mafunzo mazito yatokanayo na uzoefu wa maisha ya jamii husika.

Ni kauli fupi yenye pande mbili za fikra, ambazo upande wa kwanza huanza upande wa pili humaliza. Kwa mfano: Mficha ugonjwa, kifo humuumbua. Mcheza kwao hutunzwa. Haraka haraka haina baraka. Mkono mtupu haulambwi. Mkamia maji hayanywi.

Kila taifa na kila kabila lina methali zake. Biblia, kwa mfano, inakusanya nyingi kati ya zile za Israeli katika kitabu maalumu, mbali ya nyingine kupatikana katika vitabu vingine, hasa vile vya hekima.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne