Mfumo radidia

Henry Moseley (1887–1915) Mkemia


Mfumo radidia (pia: jedwali la elementi, en:Periodic table of elements) ni mpangilio wa elementi za kikemia kufuatana na namba atomia. Mpangilio huanza na namba ndogo. Namba atomia yatokana na idadi ya protoni katika kiini cha atomi.

Elementi hupangwa kwa radidi (periodi) na makundi.

Kuna radidi 7 zinazoonekana kama mstari wa kulala katika mpangilio huo. Kati ya radidi saba radidi na. 1 ina elementi mbili tu yaani hidrojeni na heli. Radidi na. 2 na radidi na. 3 zote zina elementi 8, kuna pia radidi kubwa zaidi.

Makundi yaonekana katika nguzo za kusimama. Kuna makundi 18. Elementi ndani ya kundi moja zina idadi sawa za elektroni za nje yaani kwenye mzingo elektroni wa nje. Kwa hiyo tabia zao zinafanana kikemia. Kwa mfano, kundi la 18 launganisha gesi zisizoathiri elementi nyingine kama vile heli, xenoni na arigoni.

Mfumo radidia ilianzishwa na wanakemia wawili mnamo mwaka 1869, ingawa Mrusi Dimitri Mendeleev (1834-1907) na Mjerumani Julius Lothar Meyer (19 Agosti 1830 - 11 Aprili 1895) walifanya kazi kila mmoja peke yake.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne