Mhunzi

Mhunzi kazini
Mhunzi (Tanzania)

Mhunzi ni mtu anayechonga vitu vya metali.

Kwa kawaida ashughulika vifaa vya chuma au feleji. Metali hupashwa mto hadi kung'aa nyekundu na kupewa umbo linalotakiwa.

Vyombo vyake ni nyundo, koleo na fuawe.

Siku hizi shughuli nyingi za mhunzi hutekelezwa kwa mashine lakini bado kuna shughuli zinazohitaji ufundi na ujuzi wa mhunzi.

Katika historia wahunzi walihitajiwa sana katika jamii kwa sababu vifaa kama silaha au majembe yalitegemea kazi ya wahunzi.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne