Mkoa wa Mwanza


Mkoa wa Mwanza
Mahali paMkoa wa Mwanza
Mahali paMkoa wa Mwanza
Mahali pa Mkoa wa Mwanza katika Tanzania
Majiranukta: 2°45′S 32°45′E / 2.750°S 32.750°E / -2.750; 32.750
Nchi Tanzania
Wilaya 8
Mji mkuu Mwanza
Serikali
 - Mkuu wa Mkoa Abas Kandoro
Eneo
 - Jumla 19,592 km²
Idadi ya wakazi (2022)
 - Wakazi kwa ujumla 3,699,872
Tovuti:  http://www.mwanza.go.tz/
Mwanza

Mkoa wa Mwanza ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania, wenye postikodi namba 33000.

Umepakana na Geita upande wa magharibi, Shinyanga na Simiyu upande wa kusini na Mara upande wa mashariki. Ziwa la Viktoria Nyanza liko kaskazini.

Makao makuu ya mkoa yapo Mwanza mjini.

Mkoa una wakazi 3,699,872 kadiri ya sensa ya mwaka 2022 [1].

Kabla ya kumegwa na kuzaa mkoa mpya wa Geita, mkoa wa Mwanza ulikuwa na wakazi 2,942,148 (sensa ya mwaka 2002) katika wilaya 8 ukiwa na eneo la 19,592 km2.

  1. https://www.nbs.go.tz

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne