Muziki

Zumari ya miaka 41,000 iliyopita iliyotengenezwa kwa mfupa.
Mchoro wa Ugiriki wa Kale juu ya chombo ukionyesha kipindi cha muziki (510 KK hivi).

Muziki ni aina ya sanaa inayotumia sauti mbalimbali: za kibinadamu na za ala za muziki, ama kwa pamoja au kila moja pekee.

Asili ya neno iko katika lugha ya Kigiriki ambamo huitwa μουσική (mousikee).

Baadhi ya sifa za muziki ni uzito wa sauti (pitch) na wizani au mahadhi (rhythm).

Aina ya muziki inayopatikana kote duniani ni nyimbo ambazo ni maneno yanayotolewa kwa sauti na mahadhi fulani mara nyingi pamoja na ala za muziki. Kwa wanaorekodi sauti, wao huenda kwa studio kurekodi na huchukuliwa kwa kinasasauti kilichoambatanishwa na tarakilishi na kudhibitiwa na kompresa.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne