Sanaa

Sehemu ya La Gioconda, mchoro wa Leonardo da Vinci unaotunzwa huko Paris (Ufaransa).

Sanaa (kutoka neno la Kiarabu) ni ufundi anaoutumia mwanadamu ili kuwasilisha fikra au mawazo yaliyo ndani ya akili yake.

Vilevile sanaa ni uzuri unaojiibua katika umbo lililosanifiwa.

Kusanifu ni kuumba, kufanya jambo au kitu kwa kutumia ufundi/ustadi ili kiweze kuvutia watu kwa uzuri wake. Mtu hueleza hisia zinazomgusa kwa kutumia umbo fulani ambalo limesanifiwa.

Hivyo kazi yoyote ya sanaa inategemewa ioneshe ufundi wa hali ya juu ili iwe na mvuto kwa hadhira yake.

Tunaweza kuona kazi ya sanaa kupitia tanzu za fasihi, uchoraji, ususi, ufumaji, utarizi, uchongaji, ufinyanzi na kadhalika.

Kila umbo huwa na nyenzo zinazotumika katika kuliumba umbo hilo. Kwa mfano katika uchongaji kuna mti (gogo), panga, tezo, msasa, rangi na kadhalika.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne