Septuaginta

Ukurasa moja wa Codex Vaticanus ambayo ni muswada ya kale kamili zaidi ya Biblia yote kwa lugha ya Kigiriki

Septuaginta (neno la Kilatini lenye maana ya "70"; kifupi LXX) ni tafsiri ya Biblia ya Kiebrania (au: Tanakh) kwa lugha ya Kigiriki ililofanywa mjini Aleksandria (Misri) kuanzia karne ya 3 KK hadi karne ya 1 KK.

Jina hilo limetokana na hadithi ya kwamba wataalamu Wayahudi 72 walitafsiri vitabu vya Torati katika muda wa siku 72 wakati wa mfalme Ptolemaio II (285–246 KK).

Idadi ya 72 ilitokana na watu sita kutoka kila moja kati ya makabila 12 ya Wanaisraeli ikafupishwa kwa kuikumbuka kirahisi kuwa "70".

Jina hilo liliendelea kutumiwa kwa tafsiri ya Kigiriki ya vitabu vyote vya Tanakh.

Wataalamu wa historia huona kwamba wakati wa Ptolemaio II vitabu vitano vya Torati (vitabu vitano ya Musa) vilitafsiriwa, na vingine vilifuata polepole katika muda wa miaka 200 hivi.

Kutokana na historia hiyo ndefu kuna tofauti katika lugha ya vitabu mbalimbali.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne