Tufani

Picha ya rada ya tufani upande wa kaskazini ya ikweta
Picha ya tufani jinsi inavyoonekana kutoka kituo cha anga

Tufani (kutoka neno la Kiarabu) ni dhoruba yenye mwendo wa kuzunguka. Inasababishwa na eneo la shindikizo duni la hewa ambako upepo umeanza kuzunguka ndani yake.

Mzunguko huu hufuata mwendo wa saa katika maeneo ya kusini kwa ikweta na huenda kinyume cha mwendo wa saa katika maeneo ya kaskazini kwa ikweta.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne