Vielezi

Mifano
  • Mary anaimba vizuri
  • Wafanyabiashara wanauza jumla
  • Ndondi si mchezo mzuri sana
  • Kidawa anatembea harakaharaka
  • Joshua anakula polepole

Kielezi (alama yake ya kiisimu ni: E, ing. adverb) ni neno au maneno yanayotoa taarifa ihusuyo kitenzi. Maneno hayo (vielezi) huelezea/hufafanua na kupambanua au kuongeza maana zaidi ya namna au jinsi tendo linavyotendeka - idadi au kiasi cha kutendeka kwa tendo hilo, mahali ambapo tendo linatendeka.

Hivyo basi kielezi ni neno au maneno yanayotoa taarifa ili kukujulisha kuwa kitenzi hicho kimetendeka namna gani au jinsi gani, mara ngapi au kwa kiasi gani, wapi, lini na kwa sababu gani.

Wakati mwingine vielezi hutoa taarifa inayohusu nomino, viwakilishi, vivumishi na hata vielezi vyenzake.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne