Waanabaptisti

Uenezi wa tapo hili katika Ulaya ya Kati miaka 1525-1550.


Waanabaptisti (kwa Kilatini anabaptista,[1] kutoka Kigiriki ἀναβαπτισμός ambapo ἀνά, ana inamaanisha "tena" na βαπτισμός, baptismos, "ubatizo"[2]) ni Wakristo ambao hasa kuanzia karne ya 16 walikataa ubatizo jinsi ulivyotolewa na Kanisa Katoliki na madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti.[3][4]

Kwa sababu hiyo, wenyewe hawapendi kuitwa hivyo: kwa mtazamo wao, hawarudii ubatizo, ila wanautoa kwa usahihi kwa mara ya kwanza.[5]

Msimamo wao ulisababisha kuanzia mwaka 1527 dhuluma kali kutoka kwa viongozi wa madhehebu hayo mbalimbali.

Kwa sasa Waanabaptisti wote hawafikii milioni 2 duniani.

  1. "Anabaptist, n.", Oxford English Dictionary, Oxford University Press, Desemba 2012, iliwekwa mnamo 21 Januari 2013{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Anabaptism, n.", Oxford English Dictionary, Oxford University Press, Desemba 2012, iliwekwa mnamo 21 Januari 2013{{citation}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. McGrath, William, "Neither Catholic nor Protestant", CBC 4 me (PDF), ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-12-27, iliwekwa mnamo 2014-08-30 {{citation}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  4. Gilbert, William, "CHAPTER 15 THE RADICALS OF THE REFORMATION", THE ANABAPTISTS AND THE REFORMATION, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-12-25, iliwekwa mnamo 2014-08-30 {{citation}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help).
  5. Vedder, Henry Clay (1905). Balthasar Hübmaier, the Leader of the Anabaptists. New York: GP Putnam's Sons.

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne