Wayahudi

Wayahudi
ethnoreligious group, Taifa, people
Native labelיהודים Hariri
Lugha zinazozungumzwa, zilizoandikwa au zilizotiwa sahihiKiebrania Hariri
DiniUyahudi Hariri
Ameitwa baada yaYuda Hariri
NchiIsrael Hariri
Taifa alipo zaliwaYuda Hariri
Studied inJewish studies Hariri
Historia ya madaJewish history Hariri
Mkabala naGentilitas Hariri
Has listlists of Jews Hariri

Wayahudi (kwa Kiebrania יְהוּדִים, Yehudim) ni kundi la kikabila na la kidini lenye asili yake katika eneo la Israeli ya Kale (Mashariki ya Karibu). Kabila la Kiyahudi, taifa la Kiyahudi na dini ya Kiyahudi, yote yana uhusiano wa karibu sana, kwa sababu Uyahudi ndio dini ya jadi ya watu wa taifa la Kiyahudi

Katika utamaduni wa Kiyahudi, ukoo unarudi nyuma hadi kwa mababu wa Biblia kama vile Abrahamu, Isaka, Yakobo na wanae 12 katika milenia ya 2 KK. Lakini tangu kale wanaogeuka kuwa Wayahudi na kuingizwa ndani ya kundi lao, hadhi yao ni sawa na wale ambao wamezaliwa ndani ya kabila hilo.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne