Wolfgang Amadeus Mozart

Wolfgang Amadeus Mozart

Wolfgang Amadeus Mozart (Salzburg, 27 Januari 1756Vienna, 5 Disemba 1791) alikuwa mtunzi mashuhuri wa opera na mpigaji wa ajabu sana wa piano kutoka nchini Austria.

Licha ya kuwa na maisha mafupi (alifariki akiwa na umri wa miaka 35 tu), alitunga zaidi ya nyimbo 800 za kila aina, zikiwemo opera (muziki wenye hadithi) Don Giovanni na Die Zauberflöte (Filimbi ya Ajabu). Watu wanaamini kwamba Mozart ni moja kati ya watunzi bora wa muda wote wa nyimbo za Ulaya, ikimpelekea mtunzi mwenzake Joseph Haydn kuandika kuwa: "kizazi kingine hakitaona talanta kama yake tena kwa karne moja".

Kazi zake alizianza na minuet (dansi) aliyoitunga akiwa na umri wa miaka minne, na alizimalizia kwa kipande chake cha mwisho, Requiem, ambacho alikiacha hajakimaliza.


From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne