Kadoko (pia: Cadoc, Cadog, Cadocus, Catawg, Catwg; 497[1] hivi - 580) alikuwa mmonaki wa Welisi, abati wa monasteri aliyoianzisha huko Llancarfan, halafu askofu anayetajwa kama mwanzilishi wa makanisa mbalimbali hata Cornwall na Bretagne [2].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi [3] na Waanglikana kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 21 Septemba[4].