Karl Rahner

Karl Rahner S.J. (5 Machi 190430 Machi 1984) alikuwa padre na mwanateolojia wa Ujerumani wa Shirika la Yesu. Pamoja na Henri de Lubac, Hans Urs von Balthasar, na Yves Congar, anachukuliwa kama mmoja wa wanateolojia wa Kikatoliki wenye ushawishi mkubwa katika karne ya 20.

Alikuwa ndugu wa Hugo Rahner, pia mwanateolojia wa Shirika la Yesu.[1]

Kabla ya Mtaguso wa pili wa Vatikani, Rahner alifanya kazi kwa karibu na Yves Congar, Henri de Lubac, na Marie-Dominique Chenu, wanateolojia walioungana na shule inayojitokeza ya mawazo ya kitekolojia iitwayo Nouvelle Théologie. Mtaguso Mkuu huo uliathiriwa na teolojia ya Rahner na uelewa wake wa imani ya Kikatoliki.[2]

  1. Sheehan, Thomas (4 Februari 1982). "The Dream of Karl Rahner". The New York Review.{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Marmion, Declan (Machi 2017). "Karl Rahner, Vatican II, and the Shape of the Church". Theological Studies. 78 (1): 25–48. doi:10.1177/0040563916681992.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne