Jamhuri ya Kiarabu ya Misri Gumhūriyyat Misr al-ʿArabiyya (Kiarabu) | |
---|---|
Wimbo wa taifa: Biladi, Biladi, Biladi (Nchi yangu, nchi yangu, nchi yangu)
| |
Mji mkuu | Cairo |
Mji mkubwa | Cairo |
Lugha rasmi | Kiarabu |
• Rais | Abdel Fattah el-Sisi |
• Waziri Mkuu | Mostafa Madbouly |
Eneo | |
• Jumla | km2 1,010,408 |
• Msongamano | 99/km2 |
PLT (PPP) | Kadirio la 2024 |
• Jumla | ▲ $2.232 Trilioni [1] |
• Kwa kila mtu | ▲ $20,799 [1] |
PLT (Kawaida) | Kadirio la 2024 |
• Jumla | ![]() |
• Kwa kila mtu | ![]() |
HDI (2022) | ▲ 0.728 |
Gini (2019) | 31.9 |
Sarafu | Pauni ya Misri (EGP) |
Msimbo wa simu | +20 |
Jina la kikoa | .eg |
Misri (kwa Kiarabu: مصر, Masr) rasmi kama Jamhuri ya Kiarabu ya Misri ni nchi iliyoko kaskazini-mashariki mwa Afrika, na sehemu ndogo kwenye Rasi ya Sinai ya Asia. Inapakana na Libya upande wa magharibi, Sudan upande wa kusini, Israeli na Ukanda wa Gaza upande wa kaskazini-mashariki, na upande wa kaskazini na Bahari ya Mediterania. Ikiwa na idadi ya watu wapatao milioni 112, inashika nafasi ya 14 kwa idadi ya watu duniani na ya tatu kwa idadi ya watu barani Afrika. Cairo ndiyo mji mkuu na jiji kubwa zaidi la Misri.
Misri inajulikana kwa ustaarabu wake wa kale, piramidi maarufu, na Mto Nile, mto mrefu zaidi duniani.