Mwaka wa Lugha wa Kimataifa

Mwaka wa 2008 umetangazwa kuwa Mwaka wa Lugha wa Kimataifa na Umoja wa Mataifa katika azimio lililopitishwa tarehe 16 Mei 2007.[1][2]

Mwaka huo, mpango wake ni kujadili mambo ya wingi wa lugha, haki za lugha zote, na mazingira ya kutumia lugha tofauti. Azimio la kutangaza mwaka huo linataja pia shida za lugha ndani ya Umoja wa Mataifa wenyewe.[3]

Shirika la UNESCO limepewa kazi ya kupanga utekelezaji wa mwaka huo, na wameufungulia rasmi kwenye Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Mama, tarehe 21 Februari 2008.[4]

  1. U.N. General Assembly, Department of Public Information, "General Assembly Proclaims 2008 International Year of Languages, in Effort to Promote Unity in Diversity, Global Understanding" GA/10592
  2. "U.N. General Assembly, Sixty-first Session, Agenda item 114, Resolution adopted by the General Assembly, 61/266. Multilingualism" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2008-12-16. Iliwekwa mnamo 2008-03-24.
  3. "Crystal. David. 2007. "What do we do with an International Year of Languages?" Paper to Unescocat, Barcelona, European Day of Languages, 26 September 2007" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2008-02-16. Iliwekwa mnamo 2008-03-24.
  4. UNESCO, "Message from Mr Koïchiro Matsuura, Director-General of UNESCO, on the celebration of 2008, International Year of Languages," Date Added: 2007-11-05 9:44 am; Updated: 2007-12-19 2:40 pm

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Nelliwinne